STAA WA LEO ni AMIR KHAN (juu pichani), ni muigizaji maarufu wa movie za kihindi nchini INDIA, kazaliwa tarehe 14 mwezi wa 3 mwaka 1965 Bombay, Maharashtra, India, mwaka 2005 alifunga ndoa na Kiran Rao ambaye wapo kwenye ndoa hadi sasa, Amir khan ana watoto watatu Ira Khan, Azad Rao Khan, Junaid Khan, Amir khan kaigiza movie zilizo tikisa dunia na kuweka rekodi za mauzo kama DHOOM 3, 3 IDIOTS, PK, GHAJINI, LIKE STARS ON EARTH na zinginezo nyingi zilizoongeza umaarufu wa muigizaji huyu,
Amir khan mpaka sasa ana utajiri wa dola millioni 180 ni kati ya waigizaji matajiri nchini India, mwaka huu 2018 anatarajia kuachia movie yake mpya inayoitwa THUGS OF HINDOSTAN aliyoigiza na AMITABH BACHCHAN, Vijay krishna acharya akiwa ndo director wa movie hiyo, nyingine zinazotarajiwa kutoka ni SALUTE itakayotoka 2019 na SARFAROSH 2 itakayotoka 2020
No comments