TRENDING POSTS

STAA WA LEO:LEROY SANE'



Mchezaji maarufu wa soka la kulipwa  "Leroy Aziz Sane'"  ndilo jina harisi alilopewa na wazazi wake, amezaliwa tarehe 11 mwezi wa kwanza mwaka 1996 ndani ya nchi ya Ujerumani mahali panapoitwa Essen, ana urefu wa mita 1.83 na uzito wa  kilogramu 75, Sane' katika uwanja anacheza eneo la kati (mildfield) au winga.

Safari ya soka ya mchezaji Sane' imeanza 2001 ambapo alicheza katika timu ya vijana wadogo (Youth Academy) Inayoitwa SG Watternscherd 09, 2005-2008 kacheza Schalke 04, 2008-2011 kacheza Bayer leverkusen na 2011-2014 akarudi kucheza Schalke 04 zote zikiwa ni timu za vijana .
Soka la kulipwa, mchezaji Sane' alianza mwaka 2014 ambapo alisaini mkataba wa kuchezea timu ya  Schalke 04, kakipiga Schalke 04 mwaka 2014 mpaka  2015 akiifungia timu hiyo jumla ya mabao 11 tangu aingie kwenye club hiyo ya Ujerumani, mwaka 2016 Sane alisaini mkataba wa kuichezea timu ya Uingereza Machester city,  mpaka sasa kaifungia magoli 20 timu hiyo.

Ungependa mwamba huyo "Leroy Aziz Sane'" akitoka Machester city timu gani itamfaa  zaidi kwa uchezaji wake akiwa dimbani.

No comments