TRENDING POSTS

JE? WAJUA: HISTORIA YA SIKUKUU YA MWAKA MPYA (NEW YEAR)




Watu wengi duniani husherekea sikukuu ya mwaka mpya japo hawafahamu kiundani zaidi kuhusu sikukuu hiyo, nikimanisha chanzo chake ni wapi hasa na ni kina nani wameanzisha ni kwa vipi sikukuu hiyo ilienea katika nchi nyingi duniani. 


Mwaka mpya husherekewa siku ya kwanza ya mwaka katika kalenda ya Gregorian ambayo ilianzishwa na papa Gregory wa 13 mwaka 1582 ikiwa na siku 365.2425 vilevile  mwaka mpya husherekewa siku ya kwanza ya mwaka na watumiaji wa kalenda ya julian ambayo hii ndio kalenda mama iliyoanzishwa na Julius Caesar mwaka wa 46 kabla ya kristo.


Wazo la kwanza la kufanya sikukuu ya mwaka mpya lilianzia nchi ya Iraq miaka 2000 kabla ya kristo ambapo mwaka mpya ulikuwa ukifanyika katikati ya mwezi wa tatu baadaye waroma wakabadili ikawa mwanzoni mwa mwezi wa tatu. baada ya kuanza kutumia kalenda ya Gregory ndipo sikukuu ya mwaka mpya ikawa inasherekewa siku ya kwanza ya mwaka.


Siku ya mwaka mpya kidini inatambulika kama siku ambayo Yesu kristu alipewa jina na kufanyiwa tohara lakini makanisa yanayoitazama siku hiyo hivyo mpaka sasa ni makanisa ya Anglikana na walutherani. Japo katika karne hii husherekewa kama sikukuu ya kuanza mwaka mpya pia hufanywa ni siku ya mapumziko katika sehemu mbalimbali duniani.

Japo nchi nyingine husherekea mwaka mpya tarehe tofauti na januari 1 kama China, Historia inaonesha mwaka mpya ndio sikukuu inayosherehekewa na watu wengi zaidi duniani kuliko sikukuu yoyote ile, husheherekewa kwa njia mbalimbali, mwaka mpya husherehekewa usiku nchi nyingi hurusha fataki angani (fire works), familia kukutana pamoja kula na kunywa kwa pamoja 


Nawatakia mwaka mpya wenye mafanikio na baraka tele.

No comments