TRENDING POSTS

STAA WA LEO:Pierre-Emerick Emiliano François Aubameyang




PIERRE EMERICK EMILLIANO FRANCOIS AUBAMEYANG




Pierre-Emerick Emiliano François Aubameyang amezaliwa tarehe 18 mwezi wa sita mwaka 1989 mahali panapoitwa Laval katika nchi ya ufaransa, ana urefu wa mita 1.87 anacheza kama mshambuliaji (Striker) akiwa dimbani, Baba yake alikuwa ni nahodha wa timu ya Taifa ya Gabon, Mama yake ni mzaliwa wa nchi ya Uhispania.


Safari ya kambumbu Pierre kaanza mwaka 2008  alipoanza kukipiga katika timu ya wakubwa Milan, 2011 akajiunga na timu ya Saint-Étienne akafunga mabao 19 na kuwa mfungaji bora wa  2013 Coupe de la Ligue, akapata umaaarufu zaidi na kuchukuliwa na timu ya  Borussia Dortmund ya ujerumani kwa paundi millioni 14. kwenye ligi ya Ujerumani aliweza kuvunja rekodi ya kuwa fowadi bora zaidi kwani aliweza kufunga magoli 141  katika mechi 213, mwaka 2018 Pierre alichukuliwa na timu ya Arsenal kwa paundi millioni 64 ikamfanya  Pierre kuwa mchezaji ghali wa Gabon kwa muda wote.


Upande wa timu ya taifa Aubameyang alikataa kuichezea timu ya taifa ya uhispania japo ana asili ya huko akajiunga na timu ya taifa ya Gabon ambayo baba yake aliwahi kuwa nahodha wa timu hiyo


No comments