STAA WA LEO: KYLIAN MBAPPE'
Kylian Mbappe' Lottin kazaliwa tarehe 20 mwezi wa 12 mwaka 1998 ndani ya jiji la Paris nchini Ufaransa, ana urefu wa mita 1.78 katika soka ni mshambuliaji (foward), baba yake na Mbappe (Wilfred Mbappe) ambaye ni kocha kazaliwa Cameroon na mama yake Fayza Lamari ana asili ya Algeria naye ni mchezaji wa zamani wa mpira wa mikono (handball).
Safari ya soka Mbappe kaanza katika timu za vijana wadogo (youth academy),ulipofika mwaka 2015 akaanza kucheza soka la kulipwa akiwa katika klabu ya Monaco ambapo aliweza kuwa mfungaji bora kwenye ligi ya Ufaransa mwaka 2016-17 alisaidia pia kuiweka kwenye nafasi ya kwanza Timu ya Monaco kwenye ligi hiyo (ligue 1).
Mwaka mmoja baadaye (2018) Mbappe alifauru kwenda PSG (Paris saint German) kwa paundi milioni 180 baada ya kucheza kwa mkopo kwa kipindi kifupi, kiasi hicho cha fedha kilimfanya Mbappe kuwa mchezaji mdogo ghali zaidi kuwahi kutokea na mchezaji wa pili ghali zaidi duniani, Mbappe amecheza kwa kujituma sana akiwa na klabu ya PSG kwani kasaidia timu hiyo kuwa nafasi ya kwanza katika ligi za ufaransa (coupa de France, Coupa de la ligue na ligue 1)
Mwaka 2017 Mbappe alianza kuchezea timu yake ya taifa (Ufaransa) ,katika kombe la dunia mwaka 2018 alionekana kuwa ndio mcheza soka mdogo toka Ufaransa kufunga kwenye kombe la dunia pia aliweza kuwa ndio mchezaji anayechipukia wa pili kufunga kwenye fainali za kombe la dunia wa kwanza akiwa ni pele'. mwisho wa kombe la dunia 2018 Mbappe' aliweza kuchukua zawadi ya mchezaji bora anayechipukia.
No comments