TRENDING POSTS

JE? WAJUA : UKWELI WA DHANA KUHUSU NYOKA

Image result for snake

Kwa kawaida nyoka hutazamwa kwa hatari kubwa, waerevu na mara nyingine hata kuhusishwa na imani potofu na uchawi katika baadhi ya jamii za Kiafrika.
Kwa kawaida nyoka anakuwa juu ya orodha ya mambo ambayo mtu anaogopa maishani mwake. Maelfu ya watu duniani hufariki kutokana na sumu kali ya nyoka baada ya kuumwa kila mwaka kwa mujibu wa shirika la afya duniani.Ukosefu wa matibabu na hata matibabu mabaya hufanya vifo hivyo kutokingika.Kuumwa na nyoka huenda kusionekane kuwa janga baya la kiafya.Lakini katika maeneo mengine duniani ni hatari kila siku na huenda kukasababisha maafa ama hata kubadilisha maisha ya mtu.Pengine ndio sababu ya kuwepo dhana tofuati, baadhi potofu, kuhusu wanyama hawa. 

Hebu tuwafahamu zaidi.

Image result for snake
Nyoka hutambaa kwenye mawe na kamba
Wanaweza kutambaa juu na hata chini ya mawe, kwenye miti na majengo. Nyoka hupenda kujificha ardhini.Ni rahisi kwao kujificha chini ya vichaka, na vigumu kutambaa chini ya mawe madogo kwenye bustani.Ni vyema kuzikata nyasi ziwe ndogo na uondoshe masalio yoyote ya nyasi zilizokatwa au majani makavu yalioangukana kujikusanya.Kadhalika ni vymea uondoshe sehemu za mti zilizoanguka juu ya paa au zinazoning'inia kutoka nyumba yako.

Image result for snake
Nyoka Mkubwa hujitenga na familia yake
Iwapo nyoka huzaa watoto au kutaga mayai, kawaida anapojifungua huwaondokea watoto na kuwaacha kivyao.Iwapo utamuona nyoka mkubwa karibu na mdogo basi huenda ni sadfa tu.Wao hutawanyika punde wanapojifungua.
Nyoka huteleza
Kawaida, watu ambao hawajawahi kumgusa nyoka hudhani kwamba wanyama hao huteleza ukiwagusa. Ngozi ya nyoka huonekana kuwa kavu, lakini kwa kuigusa ni nyororo.
Nyoka huogopa binadamu
Nyoka wanaogopa binaadamu zaidi ya binaadamu wanavyowaogopa. Kwa kawaida huwa wana haya au aibu sana na iwapo wangekuwa na nafasi anaweza kutoroka asionekane.Ni iwapo tu amekwama au ametishiwa, kama ilivyo kwa kiumbe chochote, nyoka hushambulia kujilinda.Lakini mara nyingi baadhi huona afadhali kutoroka kuliko kushambulia.
Sio  Nyoka wote hutaga mayai
Licha ya kwamba reptilia wengi hutaga mayai, sio nyoka wote wanaotaga. Baadhi ya nyoka kama wa aina ijulikanayo kama Oriental Vine, huzaa nyoka wadogo.

Image result for oriental  vines snake baby

Image result for snake eggs




No comments