TRENDING POSTS

JE ? WAJUA : HISTORIA YA SIKU YA WAPENDANAO ( VALENTINE DAY )

Image result for valentine's day


Hadithi zilizosababisha sikukuu kuenea

Siku ya wapendanao (kwa KiingerezaValentine's Day) ni sikukuu ambayo huadhimishwa kila ifikapo tarehe 14 Februari ya kila mwaka.
Historia yake imeanzia karne ya 3 huko Roma ambapo alikuwapo padri Valentinus ambaye akaja kuheshimiwa kama mtakatifu hasa tarehe hiyo.


Inasemekana kwamba Kaisari wakati huo alikuwa Claudius II: yeye aliona kuwa askari mkakamavu na bora zaidi ni yule asiyeoa wala kuwa na familia (kapera). Hivyo alipiga marufuku ndoa kwa askari.


Valentinus alipinga jambo hili na hivyo kuendelea kufungisha ndoa kwa siri. Mfalme Claudius alipopata habari hizi aliamuru Valentinus akamatwe na kuuawa.


Kuna hadithi nyingine ya kuwa akiwa gerezani Valentinus aliandika barua ambayo ilikuwa na salamu za kwanza za Valentine kwa binti aliyekuja kumsalimia gerezani; mwisho wa barua alihitimisha kwa maneno haya: Kutoka kwa Valentinus wako.


Toka hapo Valentine anakumbukwa kama mtetezi wa wapendanao na sikukuu yake kuadhimishwa kote duniani.

No comments