STAA WA LEO : WIZKID
Ayodeji Ibrahim Balogun (amezaliwa 16 Julai, 1990), anafahamika zaidi kwa jina lake la kisanii kama Wizkid (wakati mwingine hupambizwa kama WizKid), ni msanii wa rekodi, mtunzi wa nyimbo na mtumbuizaji kutoka nchini Nigeria. Alianza kazi ya muziki akiwa na umri wa miaka 11, na kutoa albamu ya ushirika akiwa na Glorious Five iliyopewa jina la Lil Prinz (2001). Mwaka wa 2009, ameingia mkataba na Banky W. iliyo chini ya Empire Mates Entertainment. Ameanza kupata umaarufu zaidi mnamo mwaka wa 2010 baada ya kutoa kibao cha "Holla at Your Boy" kutoka katika albamu yake ya kwanza iliyoitwa Superstar (2011). "Tease Me/Bad Guys", "Don't Dull", Gidi Girl, "Love My Baby", "Pakurumo" na "Oluwa Lo Ni" zilikuwa single kutoka katika albamu ya Superstar. Albamu yake ya pili iliyoitwa , Ayo (2014), ilitanguliwa na vibao kama vile "Jaiye Jaiye", "On Top Your Matter", "One Question", "Joy", "Bombay" na "Show You The Money". Kwa zaidi, katika kazi za kujitegemea, Wizkid amepata kushirikiana na baadhi ya wasanii ambao wamo katika kazi kama vile "Girl" (Bracket), "Fine Lady" (Lynxxx), "Sexy Mama" (Iyanya), "Slow Down" (R2Bees), "The Matter" (Maleek Berry), "Pull Over" (Kcee) na"Bad Girl" (Jesse Jagz).
Kazi na mchango wake katika Tasnia ya Muziki wa Nigeria umepelekea kupata mafanikio kadha wa kadha, ikiwa ni pamoja na tuzo ya BET Award, a MOBO Award, The Headies Awards tatu, Channel O Music Video Awards mbili, nne za Nigeria Entertainment Awards, Ghana Music Award, mbili za Dynamix All Youth Awards, mbili za City People Entertainment Awards, na Future Award. Kwa zaidi, amepata kuchaguliwa mara tatu katika MTV Europe Music Awards vilevile mara nne katika tuzo za World Music Awards. Alipata kuwa nafasi ya 5 kwa msanii mwenye pesa sana wa Afrika mwaka 2013 na jarida la Forbes na Channel O. Mnamo Februari 2014, Wizkid amekuwa mwanamuziki wa kwanza wa Kinigeria kuvuka idadi ya milioni 1 ya watu wanaomfuta katika mtandao wa Twitter
No comments