STAA WA LEO: MICHAEL DAPAAH
Nadhani wengi tutakua tunamfahamu huyu jamaa (pichani) japo sio kiundani zaidi, anaitwa Michael daapah, wengi wanamfahamu kwa jina la Big shaq au Roadman Shaq, kazaliwa mwezi wa kwanza mwaka 1991 ndani ya jiji la London nchini uingereza, Michael Dapaah sio tuu ni rapa pia anafanya sanaa ya uigizaji, ameigiza filamu za comedy kama vile somewhere in London (SWIL),ni comedy ambayo ilipata watazamaji wengi kwenye mtandao wa YOUTUBE.
Michael Dapaah alitambulika sana na watu wa uingereza alipofanya mahojiano na watangazaji wa Charlie Sloth BBC radio 1xtra "redio ya uingereza" katika kipindi kinachoitwa "Fire in the Booth", ambapo Michael Dapaah aliimba rap comedy akiimba mistari ya Man's not hot kabla haijatolewa.
Mwaka 2017 tarehe 22 mwezi wa tisa Man's not hot ilitolewa rasmi baada ya kupendwa sana na wasikilizaji wa redio wa uingereza hiyo ilipelekea Michael Dapaah kupata umaarufu duniani kutokana na style ya kipekee ya kurap ikiambatana na ubunifu mkubwa katika nyimbo ya MAN'S NOT HOT.
redio ya uingereza
No comments