TRENDING POSTS

STAA WA LEO : BRIAN DEACON


Brian Deacon - An English actor Born:... - Habeshas Network ...

Brian Deacon ndio jina lake mwigizaji huyo ambaye ni mwingereza aliyezaliwa mnamo tarehe 13/02/1949 huko Oxford nchini Uingereza akiwa ni mtoto wa pili katika familia yao, Baba yake akiwa fundi makenika na mama yake akiwa ni nesi,  ndoa yake ya kwanza na Rula Lenska ilivunjika ambapo alizaa na mkewe huyo binti yao aitwaye Lara Deacon,ndoa yake ya pili alioana na mwanamama Natalie Bloch mnamo mwaka 1998 mpaka sasa wapo kwenye ndoa hiyo.

Aliigiza filamu ya Yesu ambayo pia ilimfanya AOKOKE  baada ya kuitazama akiwa na miaka 30.Alipita kwenye mchujo mkali wa waigizaji zaidi ya elfu moja ambao walifanyiwa mahojiano huku 260 wakijaribishwa kuigiza(screen test)kuona kwamba wanafaa akiwa ni mwingereza pekee kati ya waigizaji Waisrael walioingia kwenye usaili huo, yeye akiwa chini ya kampuni iitwayo New shakespears ambako alikuwa akifanya sanaa za majukwaani na uigizaji.


Amesema kabla ya kuchaguliwa, mtihani wake wa kwanza ulikuwa kutoka kwa wakala wake aliyemvunja moyo kwa kumweleza hadhani kama yeye(Brian)atafaa kwenye kumwigiza Yesu. Baada ya hapo akawa na wakati mgumu kutoka kwa watu ambao kila mmoja alikuwa anajaribu kumweleza jinsi anavyotakiwa kuigiza,sauti yake na mambo mengine,ingawa yeye alisema atatumia sauti yake na maelezo kutoka kwa muongozaji.Amesema wiki tatu kabla hawajaanza kurekodi filamu hiyo, alisoma kitabu cha Luka mtakatifu zaidi ya mara 20 kwakuwa filamu hiyo imenukuliwa kutoka kitabu hicho, na kusoma kwake anasema kulimpa nguvu sana na moyo wa kuigiza filamu hiyo baada ya kuweza kumfahamu vyema Yesu kuwa ni mtu wa aina gani toka kitabu icho.

Katika miezi saba waliyochukua kuigiza filamu hiyo Brian amesema,walikuwa wanaigiza kwa masaa mengi kuanzia saa kumi za alfajiri mpaka mwisho wa siku kiasi kwamba wakati mwingine aliwaambia wenzake kwamba wamsaidie kwani  amechoka sana na hajui kwamba angeweza kuigiza kwa siku hiyo lakini anasema alikuwa anashangazwa na nguvu za ajabu alizokuwa akizipata na kuendelea kuigiza ingawa wakati huo anasema alikuwa mkristo kwa jina wa dini/dhehebu kubwa sana na karne kadhaa duniani, lisiloamini ktk Wokovu duniani ktk Yesu. Siku moja wakati anaigiza alikuwa anawaombea watu mara mwanamke mmoja alishika mkono wake kumbe alikuwa na mapepo, alimuombea na mapepo yalimtoka mwanamama huyo.


Siku nyingine waliokuwa wakiigiza kama wanafunzi wa Yesu( Brian) wapatao 12, wakiwa ndani ya basi walikuwa wamepanga kugoma kutokana na malipo waliyokuwa wakipata,  Brian anasema director alikuja kumuomba yeye,  azungumze nao warejee kazini,baada ya masaa 36 ya mazungumzo walikubali kurudi kuendelea na kazi


Amesema mtihani mwingine ni siku alipokuwa hotelini Tel Aviv ghorofa ya 18 usiku mara kukawa na moto hotelini hapo baada ya mwingereza mmoja aliyekuwa akivuta sigara kusahau kuizima hivyo kusababisha moto,lakini anasema bahati nzuri hakuna aliyejeruhiwa ila walifanya kazi siku inayofuatia muda mrefu bila muongozaji kujali kwamba hawakulala vyema usiku.

1 comment: